Saturday, August 31, 2013

UBUNIFU UNAVYOWEZA KUWA AJIRA YA KUDUMU:Sehemu ya 1

Leo nakuja na mada ambayo kwa namna moja au nyinginne inaweza kusaidia au kuchangia kwa kiasi fulani kukujengea wazo jipya katika akili yako. kwa kawaida watu wengi hasa vijana huwa wanaomba Mungu awasaidie wapate ajira baada ya kumaliza masomo yao ya ngazi fulani. Ni kweli, lakini lengo hasa la elimu tunayoipata mashuleni nizaidi ya ajira tunazotegemea kuajiriwa sehemu katika maofisi.
kuna kitu kinaitwa kujiajiri, na kujiajili huku kunaweza kutiwa changamoto na elimu tuliyo ipata mashuleni, yaani elimu yako ikawa ndiyo msingi wa ajira yako na ya watu wengine Yaani wewe ukasaidia watu wengine kupata ajira ndani ya ajira yako.
Mbali na elimu uliyoipata shuleni lakini pia kuna vipaji ambavyo kwavyo unaweza kuvitumia na vika yabadilisha maisha yako na ya watu wengine.

MAMBO UNAYOWEZA KUYAFANYA NA YAKABADILISHA MAISHA YAKO

1  ubunifu wa kuandaandaa keki za harusi

Unaweza ukatumia fursa hii na ukajikuta unapata mafanikio makubwa, hii ni kutokana na kuwa harusi, birthday na shuguli nyingine zinazo endana na hizo kufanyika mara kwa mara. Unaweza kuwa unatengeneza keki na hatimaye kujifatia faida kubwa, na hatimaye kuja kumiliki kampuni yako ya maswala hayo

MIFANO YA KEKI 

 

 

 

 

 

 

  

Hii ni sehemu ya kwanza ya kuzionesha fursa za mafanikio kwa kutumia ubunifu kutokana na elimu tulizozipata mshuleni, nakuepuka kukaa tukisubiri kuajiriwa na kuchelewesha maendeleo yetu sisi wenyewe
Fulsa ziko nyingi ila leo tumeanza na hii ya utengenezaji wa keti za sherehe mbali mbali
Tutaendelea na mada hii wiki ijayo
Nahitaji maoni yako ili kuboresha huduma zetu

ANGALIZO
Ili uendelee kufanikiwa katika shughuli hii anayo taka kuianzisha lazama uwe mwaminifu katika mambo yafuatayo.
1. uaminifu wa kutoa fungu la kumi (Zaka)
2. kusaidia wasiojiweza
3 kusoma neno
4. kufunga na kuombea kazi yako
5. kufanya kazi kwa bidii  
6. kupangilia matumizi ya fedha unayoipato
7. Kuweka akiba
8. Kuepuka kukatishwa tamaaa.

"Twayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu"

Its me Souzy Rajab
C.E.O SORAMA visions
           

No comments:

Post a Comment