Friday, September 13, 2013

UBUNIFU UNAVYOWEZA KUWA AJIRA YA KUDUMU. Sehemu ya 2

Sehemu ya kwanza niliianza mada hii na kuelezea jinsi ambavyo ubunifu unavyoweza kugeuka na kuwa ajira ya kudumu hasa mtu akitumia fursa za maendeleo alizo nazo 
leo nitaendelea na sehemu ya pili ya mada hii

MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA NA YAKABADILISHA MAISHA YAKO

2. Ubunifu wa utengenezaji wa baitiki

hii ni fursa ambayo imetumiwa na wanawake wengi wanaopenda maendeleo. Wanawake wengi wameingia katika kujifunza utengenezaji wa batiki na kujikuta wamepata mafanikio makubwa na kubadilisha maisha yao. Vile vile wewe kama mama, baba, kijana au binti unaweza kutumia fursa hii na kujiwekea mazingira mazuri ya kibiashara.
Ushauri wangu ni kwamba kama unapenda kujifunza utengenezaji wa batiki penda kuhudhuria semina mbalimbali zinazotoa mafundisho hayo ya utengenezaji wa batiki, vile vile tafuta marafiki wenye ujuzi huo na pia soma vitabu, vipeperushi na mitandao kama ukiweza ili kuongeza maarifa zaidi

MFANO WA BATIKI 

Photo 

Photo 

Photo 

Photo 

Photo 
Huyu ndiye dada yangu wa ukweli Ruth Nixon aliye nihamasisha niwaletee mada hii kutokana na uchapakazi wake, na ndiye aliye tengeneza batiki hizo hapo juu!
ukimuhitaji akufundishe wasiliana naye 
0769 063837 au 
facebook Ruth Nixon

 Leo naishia hapo tukutane tena wakati mwingine

Kwa habari za kupendeza endelela kutembelea blog yetu

 Its me Souzy Rajab, C.E.O SORAMA visions


No comments:

Post a Comment