Mpendwa msomaji wa blog hii leo nataka niongee na wewe kuhusu KIPAJI wengi hatuna uelewa mzuri juu ya vipaji tulivyo navyo. Sasa basi ungana na mimi ili upate kujua zaidi habari hii si ya kukosa endelea kutembelea blog hii.
Kama nilivyo kueleza hapo awali kuwa kipaji kinaweza kukutoa, na hii na maanisha kukutoa kimaisha
Je utagunduaje kama unakipaji?
Nirahisi sana , kwanza kabisa angalia kitu au vitu unavyopenda kufanya kila siku. Mfano vitu vifuatavyo
1 Kuimba
Je unapenda kuimba au napenda kusikiliza nyimbo za waimbaji mbalimbali? hutumia muda wako mwingi kwa kuimba? au kutafuta habai mbalimbali za waimbaji? kama jibu ni ndiyo basi wewe unakipaji cha uimbaji na hapo unachotakiwa kufanya ni kuanza kuchukua hatua ya kukuza kipaji chako kwa kufanya mazoezi ya kuimba na kutafuta wataalamu mbali mbali ili wakusaidie kufikia malengo yako.
2. ubunifu wa mavazi
Kama unajua una mapenzi makubwa na masuala ya mitindo, unaweza kujikita zaidi katika sehemu hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa bidii paka ikuletee mafanikio, kwa hili pia unaweza kujifunza kutoka kwa wanamitindo mbalimbali ambao tayari wameshabobea kwenye masuala haya ya mitindo. Kinachotakiwa ni kuchukua hatua na kufanya kazi kwa bidii iwezekanavyo, huku ukijifunza kwa waliofanikiwa
3. Michezo mbalimbali
kama wewe unapenda michezo, basi michezo ndiyo inaweza kukutoa kimaisha na hatimaye kufanikisha malengo yako. kinachotakiwa nikufanya mazoezo na kutafuta vikundi vya kushirikiana navyo bila woga.
Je bado hujapata wazo katika kikitumia kipaji chako?
No comments:
Post a Comment