Friday, September 13, 2013

UBUNIFU UNAVYOWEZA KUWA AJIRA YA KUDUMU. Sehemu ya 2

Sehemu ya kwanza niliianza mada hii na kuelezea jinsi ambavyo ubunifu unavyoweza kugeuka na kuwa ajira ya kudumu hasa mtu akitumia fursa za maendeleo alizo nazo 
leo nitaendelea na sehemu ya pili ya mada hii

MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA NA YAKABADILISHA MAISHA YAKO

2. Ubunifu wa utengenezaji wa baitiki

hii ni fursa ambayo imetumiwa na wanawake wengi wanaopenda maendeleo. Wanawake wengi wameingia katika kujifunza utengenezaji wa batiki na kujikuta wamepata mafanikio makubwa na kubadilisha maisha yao. Vile vile wewe kama mama, baba, kijana au binti unaweza kutumia fursa hii na kujiwekea mazingira mazuri ya kibiashara.
Ushauri wangu ni kwamba kama unapenda kujifunza utengenezaji wa batiki penda kuhudhuria semina mbalimbali zinazotoa mafundisho hayo ya utengenezaji wa batiki, vile vile tafuta marafiki wenye ujuzi huo na pia soma vitabu, vipeperushi na mitandao kama ukiweza ili kuongeza maarifa zaidi

MFANO WA BATIKI 

Photo 

Photo 

Photo 

Photo 

Photo 
Huyu ndiye dada yangu wa ukweli Ruth Nixon aliye nihamasisha niwaletee mada hii kutokana na uchapakazi wake, na ndiye aliye tengeneza batiki hizo hapo juu!
ukimuhitaji akufundishe wasiliana naye 
0769 063837 au 
facebook Ruth Nixon

 Leo naishia hapo tukutane tena wakati mwingine

Kwa habari za kupendeza endelela kutembelea blog yetu

 Its me Souzy Rajab, C.E.O SORAMA visions


Tuesday, September 3, 2013

MJUE MTUMISHI WA MUNGU ISAYA PAUL MWENYE NDOTO ZA KUIHUBIRI INJILI KIMATAIFA K

Najua hili litakuwa ni jina geni masikioni mwa wasomaji wengi wa blog hii. Lakini ni kwamba, Huyu ni mtumishi wa Mungu anayetumika katika kuihubiri injili ya Kristo kwa kufungua roho zikizofungwa na mizimu na maagano yaliyowafunga watu wengi. Mtumishi huyu anaye chukua shahada yake ya kwanza ya Elimu (BA-ED) katika chuo kikuu cha Tumaimi tawi la Dar es Salaam, amefanyika baraka kwa wanachuo wa chuo hicho na hasa baada ya kufanikisha kuanzishwa kwa tawi la (USCF) chuoni hapo. Amekuwa mstari wa mbele katita kuihubiri injili ya kweli ya Kristo na kuwaleta watu wengi kwa Yesu. Zaidi ya hayo ni kwamba mtumishi huyu anandoto za kuwa muhubiri wa kimataifa, na ameanza program ya kutengeneza CD zake za mahubiri ili kuwafikia watu wengi zaidi. 

KILA LA KHERI MTUMISHI

Photo: UKISHINDA SIKU NZIMA BILA KUTENDA DHAMBI MSHUKURU MUNGU KWA SABABU WAPO WATU WAMEFUNGWA NA NGUVU ZA GIZA NA WANATAMANI KUACHA LAKINI WANASHINDWA KABISA
FIKIRIA WAVUTA BANGI
FIKIRIA WALEVI
MAKAHABA NA WAZINZI 
FIKIRIA WANAOTESWA NA NGUVU ZA MAJINI NA MAPEPO 
WENGINE HAWALALI KABISA 
KUNA WATU WANAONA MATESO NI SEHEMU YA MAISHA YAO WAMETUMIA AKILI ZAO  NA WAMESHINDWA
FIKIRIA MTAANI KWAKO VILE UOVU UNAVYOZIDI 
NI KWA NEEMA TU WEWE UPO HIVO  WALA SI UJANJA WAKO NAKUARIKA KUOMBEA TAIFA HILI MAANA MUNGU WETU ALIYEJAA UZIMA YU HAI YEYE NI WA HURUMA OMBEA TAIFA HILI OMBEA VIJANA MAANA SIKIO LA BWANA YESU LI NAKUSIKIA SASA 

Mttumishi wa Mungu Isaya Paul.

Its me C.E.O SORAMA visions

Monday, September 2, 2013

ZANELE FROM SOUTH AFRICA.

Nimevutiwa na mshono wake! nani anaweza kunishonea kama huu? Tuwasiliane humu humu au fb. 

 

Love you all  my friends, Its me C.E.O SORAMA visions!

PIC OF THE DAY.

MR AND MRS MBATHA 

 
Watumishi wa Mungu Mr. Nqubeko Mbatha na Mkewe Ntokozo Mbambo. Wote wanamtumikia Mungu huko South Africa kwa njia ya uimbaji.
Wamejaaliwa watoto wakike wawili.
Wote wametokea katika kundi kubwa la Muziki wa Injili la Joyous Celebration
Kabla ya kuwa waimbaji wa kujitegemea.